Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia imefanya mazungumzo na Somaliland kuhusu ushirikiano wa kijeshi

Somaliland Ethiopiaaaa.png Ethiopia imefanya mazungumzo na Somaliland kuhusu ushirikiano wa kijeshi

Tue, 9 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Nchi ya Ethiopia, imesema imefanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa kijeshi na viongozi wa Somaliland, ikiwa ni wiki moja tangu pande hizo zitiliane saini mkataba wa matumizi ya bahari yake, hatua iliyoibua mzozo mpya wa kikanda.

Majadiliano ya hapo jana, yamefanyika wakati ambapo rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud aakianza ziara katika nchi jirani ya Eritrea.

Somalia inatafuta uungwaji mkono wa kimataifa kuhusu makubaliano ya Januari Mosi mwaka huu yenye utata kati ya Ethiopia na Somaliland -- eneo lililojitangaza kujitenga licha ya upinzani wa Mogadishu.

Mogaidishu imeyataja makubaliano ya juma lililopita ambayo yanaipa haki Ethiopia isiyo na bandari kutumia eneo la Bahari Nyekundu kupitia Somaliland, kama "uchokozi" na ukiukaji wa uhuru wake.

Licha ya wasiwasi wa ukanda na jumuiya ya kimataifa kuhusu mkataba huo, mkuu wa jeshi la Ethiopia Birhanu Jula na mwenzake wa Somaliland Nuh Ismail Tani, walikutana jana, kulingana na taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook wa jeshi la Ethiopia.

Haya yanajiri wakati huu waziri wa ulinzi wa Somaliland, akitangaza kujiuzulu kwenye nafasi yake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live