Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia: Zaidi ya watu 400 wamefariki kutokana na njaa Tigray

Njaa Yaua Watu 50 Nchini Ethiopia Huku Kukiwa Na Ukame Ethiopia: Zaidi ya watu 400 wamefariki kutokana na njaa Tigray

Wed, 31 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu zaidi ya 400 nchini Ethiopia, kwenye jimbo la Tigray na Amhara, wamefariki kutokana na njaa katika miezi ya hivi karibuni, imesema ripoti ya tume ya haki za binadamu nchini humo.

Taarifa hii ya taasisi ya kuchunguza malalamishi ya raia, inakuja huku mamlaka za maeneo hayo zikishikilia msimamo kuwa hakuna aliyekufa kutokana na njaa eneo hilo.

Taasisi hiyo imesema tathmini ya watalaam wao imebainisha kuwa mamilioni ya raia kutoka majimbo hayo mawili wameathirika, huku maelfu ya watu wakiwa wamefurushwa kwenye makazi yao.

Mkuu wa taasisi hiyo Endale Haile amesema vifo vya aina hiyo vimetokea katika miezi sita iliyopita na kuna maelfu ya watoto kutoka maeneo hayo ambao hawajakuwa wakienda shuleni.

Taasisi hiyo imetoa wito kwa mashirika ya serikali kutopoteza muda zaidi kuhusu hali hiyo na baadala yake kuanza utoaji msaada.

Juma lilopita ofisi ya mawasiliano wa utawala wa majimbo hayo ilisema kulikuwa na watu milioni sita wanaohitaji msaada wa dharura kwa sababu ya athari za ukame.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live