Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia: Waziri Mkuu amewaonya wanaotishia uhuru wa nchi yake

Bw Abiy Ethiopia: Waziri Mkuu amewaonya wanaotishia uhuru wa nchi yake

Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ameonya kwamba nchi yake itakabiliana na taifa lolote linalotishia uhuru wa nchi yake.

Abiy amesema hapatakuwa na mazungumzo yoyote kuhusu uhuru wa taifa lake na kwamba nchi yake iko tayari kukabiliana na adui wa aina yoyote, kauli iliotoa wakati wa siku ya Uhuru.

Kauli ya Abiy, ametoa wakati huu taharuki ikiendelea kushuhudiwa kati ya nchi yake na Somalia ambayo imeendelea kupinga hatua ya Ethiopia kusaini mkataba wa kutumia bandari ya jimbo linalojitawala la Somaliland, Somalia ikisitiza jimbo hilo bado ni sehemu ya himaya yake.

Taifa la Ethiopia ambalo pia ni taifa la pili kwa ukubwa barani Afrika, pia lipo kwenye mzozo na taifa jirani la Misri na Sudan ambazo zinapinga hatua ya Ethiopia, jenga bwawa na kulijaza kwa kutumia maji ya Mto Nile.

Mwezi uliopita Ethiopia ilisema baadhi ya watu wanalenga kutatiza usalama wa kikanda, baada ya Misri kutuma zana za kivita nchini Somalia, Misri pia ikipanda kutuma wanajeshi wake nchini Somalia kujaza nafasi ya wanajeshi wa ATMIS, ambao Ethiopia ina idadi kubwa katika kikosi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live