Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia: Wakomba mamilioni benki baada ya hitilafu ATM

Benki Mamilioni.png Ethiopia: Wakomba mamilioni benki baada ya hitilafu ATM

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Benki kubwa ya biashara nchini Ethiopia inajitahidi kurejesha kiasi kikubwa cha fedha kilichochotwa na 'wateja' baada ya kutokea shida kwenye mfumo wa kutoa fedha.

Wateja hao waligundua mapema juzi kwamba kulikuwa na shida kwenye mfumo na hivyo wangeweza kuchukua pesa taslimu zaidi ya walizokuwa nazo kwenye akaunti zao katika Benki ya Biashara ya Ethiopia (CBE).

Ilichukua saa kadhaa kabla ya benki hiyo kugundua tatizo na kusimamisha mfumo wa kutoa fedha kupitia mashine (ATM).

Inasemekana waliochota pesa nyingi kutoka benki ya CBE inayomilikiwa na serikali ni wanafunzi, Rais wa benki hiyo, Abe Sano amewaambia waandishi wa habari na kutaka wahusika warudishe fedha hizo.

Amesema habari za hitilafu za mashine zilienea haraka katika vyuo vikuu kwa kupitia programu za ujumbe wa simu, hali iliyosababisha mistari mirefu iliyoundwa kwenye ATM, hususani katika chuo kikuu kimoja kilichopo magharibi mwa Ethiopia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live