Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia: Serikali yakanusha ripoti kuwa maofisa wake waliwaua raia Amhara

Amhraa Ethiopiaaaaaaaaa.png Ethiopia: Serikali yakanusha ripoti kuwa maofisa wake waliwaua raia Amhara

Fri, 16 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Serikali ya Ethiopia imekanusha madai kuwa, wanajeshi wake waliua raia wengi mwezi uliopita katika eneo lenye machafuko la Amhara, wakati huu mataifa ya Magharibi yakitaka uchunguzi huru kufanyika kuhusu mauaji hayo.

Uasi kwenye eneo la Amhara - jimbo la pili kwa ukubwa nchini Ethiopia – ulizuka mwaka jana wakati serikali ilipochukua hatua ya kufuta vikosi vya kikanda na kuviingiza katika jeshi la kitaifa.

Watetezi wa haki wamebainisha aina mbalimbali za ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na vikosi vya serikali katika eneo hilo, ikiwa ni pamoja na madai ya mauaji ya kiholela na ubakaji.

Kauli ya serikali inakuja siku chache kupita tangu tume huru ya haki za binadamu nchini humo, idai kuwa wanajeshi wa Serikali waliua zaidi ya raia 45 kwenye jimbo hilo, huku mashirika mengine yakidai ni zaidi ya 80.

Jumatano ya wiki hii, Uingereza ilitoa wito wa uchunguzi kuhusu matukio ya Merawi, siku moja baada ya Umoja wa Ulaya kutoa wito wa uchunguzi na mazungumzo kutatua mzozo wa Amhara.

Wapiganaji wa Fano, ambao walishirikiana na Serikali katika vita ya Tigray, wamekuwa hawana uhusiano mzuri na utawala wa Addis Abab, tangu kundi la wapiganaji wake kuvunjwa, Amhara kwa sasa ikisalia chini ya makataa ya Hali ya dharura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live