Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia: Mazungumzo kati ya wapiganaji wa TPLF na serikali yameanza

Ethiopiaaaaa Mazungumzooo.png Ethiopia: Mazungumzo kati ya wapiganaji wa TPLF na serikali yameanza

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wawakilishi kutoka serikali kuu ya Ethiopia na wale wa jimbo la Tigray wameanza mazungumzo mjini Addis Ababa, kujaribu kumaliza ucheleweshaji wa utekelezaji wa makubaliano ya amani ya Pretoria.

Muafaka wa Pretoria unalenga kutatua baadhi ya masuala ikiwemo ugawaji wa madaraka, uthibiti wa rasilimali pamoja na kutatua changamoto ibuka kwa njia ya mazungumzo.

Kumekuwepo na hali ya wasiwasi kuhusu utekelezwaji wa vipengele vya mkataba huo, hatua ambayo iliufanya Umoja wa Afrika kuingilia kati.

Haya yanajiri wakati huu Getachew Reda, rais wa mpito katika jimbo la Tigary akieleza kuwa hakutakuwepo mazungumzo mengine kabla ya kutekelezwa kwa agenda ambazo bado hazijatatuliwa.

Mazunguzmo hayo yanaongozwa na rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta na rais mstaafu wa Nigeria wa Olusegun Obassanjo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live