Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ethiopia: Kujaza maji Bwawa la Renaissance si kipaumbele tena

Bw Abiy Ethiopia: Kujaza maji Bwawa la Renaissance si kipaumbele tena

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, amesema kwamba suala la kujaza maji katika Bwawa la Renaissance sio kipaumbele tena kwa nchi yake ambayo imehifadhi maji ya kutosha na kwamba misri haijapatwa na madhara yoyote kutokana na suala hilo kama ilivyokuwa ikivumishwa hapo awali.

Abiy Ahmed, ambaye jana alikuwa akihutubia Bunge la Ethiopia, amesisitiza kuwa serikali yake iko tayari kwa mazungumzo yatakayodhamini maslahi ya pande zote.

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema: "Tutawasikiliza ndugu zetu wa Misri na kubadilishana nao mawazo, na tutajibu wasiwasi wao."

Ameeleza kuwa ingawa chanzo cha Blue Nile kiko Ethiopia, lakini Addis Ababa haijaingiza siasa katika suala hilo, "badala yake, iko tayari kugawana rasilimali zake na wengine, na Mto Nile bado unatiririka kwa majirani zetu na hautakoma".

Ikumbukwe kwamba mwezi Disemba mwaka jana, mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ulishuhudia mkutano wa nne na wa mwisho kati ya Ethiopia, Misri na Sudan kuhusu Bwawa la Renaissance linalojengwa na Ethiopia juu ya maji ya Mto Nile, ambapo Cairo ilitangaza baadaye katika taarifa ya mwisho kwamba mazungumzo kuhusu bwawa hilo yamegonga mwamba. Bwawa la Renaissance

Ujenzi wa Bwawa la Renaissance juu ya maji ya Mto Nile huko Ethiopia umeibua mvutano mkubwa wa maji kati ya nchi hizo tatu tangu mwaka 2011 hadi sasa.

Misri na Sudan zinahofia bwawa hilo kubwa lililoghrimu dola bilioni 4.2 litapunguza kwa kiasi kikubwa sehemu ya maji ya Mto Nile wanayopokea, na mara kadhaa zimeiomba Addis Ababa isitishe kulijaza hadi makubaliano yafikiwe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live