Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eswatini yakanusha madai kuwa inakabiliwa na upungufu wa wanaume

Mwanasiasa Wa Upinzani Nchini Eswatini Auawa Kwa Kupigwa Risasi Eswatini yakanusha madai kuwa inakabiliwa na upungufu wa wanaume

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ufalme wa Eswatini umekanusha ripoti kuwa unatoa uraia kwa watu kutoka nchi za kusini mwa Afrika kujaza nafasi ya uhaba wa wanaume kwenye taifa hilo.

Hatua hii imekuja baada ya kusambaa kwa barua iliodaiwa kuandikiwa na mfalme Mswati III akielezea kuguswa na upungufu wa wanaume kwenye ufalme wake.

Kwa mujibu wa barua hiyo ambayo mamlaka inasema ni feki, iliadai kuwa mfalme alikuwa tayari kuwafadhili wanaume kutoka kusini mwa Afrika wenye nia kuwaoa wanawake kutoka nchini mwake ambapo pia wamengepewa nyumba bila malipo.

Haijabainika ni nani aliyechapisha barua hiyo ambayo ilionekana kuwafuraisha baadhi ya watumiaji ya mitandao ya kijamii kutoka kusini mwa Afrika.

Eswatini, nchi peke ambao kwa sasa ndio bado inaoongozwa na wafalme barani Afrika, ina idadi ya watu milioni 1.2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live