Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Estonia kufungua ubalozi Nairobi

E186ec6bb8738e362650876b2acae39b Estonia kufungua ubalozi Nairobi

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

ESTONIA inapanga kufungua ubalozi wake katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi mwakani.

Ubalozi huo utakuwa ni wa pili wan chi hiyo barani Afrika, wa kwanza ukiwa nchini Misri ambao umekuwa ukifanya kazi tangu 2010.

Mpango wa kufungua ubalozi huo mpya ulibainishwa katika mpango Estonia kwa Afrika katika kipindi cha 2020-2030.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Kenya inakusudia kusaidia wanadiplomasia wa Estonia katika kugombea huduma ya mambo ya nje katika Jumuiya ya Ulaya barani Afrika, kuimarisha ubadilishanaji wa wanadiplomasia na nchi nyingine wanachama na kuongeza ushiriki wa Estonia barani Afrika.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Estonia pia inakusudia kupanua mtandao wa mabalozi wa heshima katika nchi za Kiafrika.

Katika nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, mabalozi wa nchi hiyo ambao sio raia wa Estonia wameteuliwa katika nchi za Ethiopia na Mali.

Chanzo: habarileo.co.tz