Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eritrea yaishutumu Marekani kwa kuwaunga mkono waasi wa Ethiopia

Eriteaaaaa Aaa Wasi Eritrea yaishutumu Marekani kwa kuwaunga mkono waasi wa Ethiopia

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Eritrea Isaias Afwerki ameishutumu Marekani kwa kuunga mkono vikosi vya Tigray wakati wa vita kaskazini mwa Ethiopia.

Katika mahojiano na vyombo vya habari vya ndani katika mji wa bandari wa Massawa, Rais Afwerki alidai kwamba makubaliano ya amani yaliyotiwa saini kati ya serikali ya Ethiopia na chama cha Tigray People's Liberation Front TPLF yaliharakishwa na Marekani ili kuwazuia waasi kushindwa katika uwanja wa vita.

Kwa mara ya kwanza alikiri kwamba mamia kwa maelfu ya watu walikufa wakati wa vita vilivyoanza Novemba 2020, ingawa hakufafanua wanajeshi wangapi wa Eritrea waliuawa wakati wa mzozo huo.

Katika matamshi ya nadra wiki iliyopita, kiongozi huyo aliyejitenga alikanusha ripoti kwamba wanajeshi wa Eritrea walifanya uhalifu wa kivita nchini Ethiopia ambako walikuwa wametumwa kupigana pamoja na jeshi la taifa la Ethiopia na wanamgambo wanaoiunga mkono serikali.

Mkataba wa amani uliotiwa saini nchini Afrika Kusini mwezi Novemba 2022 ulimaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miaka miwili vilivyoua makumi kwa maelfu na kuwaacha mamilioni ya watu nchini Ethiopia wakihitaji msaada wa kibinadamu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live