Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eritrea yaanza mashambulizi makubwa eneo la Tigray nchini Ethiopia

Wanajeshi Elitria Eritrea yaanza mashambulizi makubwa eneo la Tigray nchini Ethiopia

Wed, 21 Sep 2022 Chanzo: BBC

Wanajeshi wa Eritrea wamefanya mashambulizi makubwa katika eneo la Tigray nchini Ethiopia, msemaji wa kundi la waasi la Tigrayan, TPLF, amesema.

Mjumbe wa Marekani alisema kuwa Marekani inafahamu kuhusu wanajeshi wa Eritrea kuvuka kuingia Tigray, na akalaani kitendo hicho.

Serikali ya Eritrea na Ethiopia bado haijatoa maoni yoyote kuhusu madai hayo.

Iwapo mashambulizi ya Eritrea dhidi ya waasi hao yatathibitishwa, itaashiria kuongezeka kufuatia kusambaratika kwa mapatano ya miezi mitano mwezi uliopita.

Mzozo ulizuka kwa mara ya kwanza mnamo Novemba 2020 kufuatia mzozo mkubwa kati ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed na Chama cha Ukombozi cha Watu wa Tigray (TPLF), ambacho kinadhibiti eneo hilo.

Eritrea iliingilia kati upande wa jeshi la Ethiopia, lakini inasemekana iliwaondoa wanajeshi wake wengi mwaka jana.

Siku ya Jumanne, msemaji wa TPLF Getachew Reda alisema mapigano makali yanaendelea katika maeneo kadhaa kwenye mpaka wa Tigray na Eritrea.

"Eritrea inapeleka jeshi lake lote pamoja na askari wa akiba. Vikosi vyetu vinalinda nafasi zao kishujaa," alisema katika ujumbe wake wa Twitter, na kuongeza kuwa wanajeshi wa Ethiopia pia wanashiriki katika mashambulizi hayo.

"Wanasikitishwa sana na tunalaani. Kuwepo kwa wanajeshi wa Eritrea nchini Ethiopia kunasaidia tu kutatiza mambo, na kuchochea hali ya kutisha," alisema.

Maelfu ya watu wameuawa na mamilioni wamekimbia makazi yao katika mzozo huo.

Ufikiaji huko Tigray umezuiliwa sana na ni vigumu kupata uthibitisho huru wa mapigano hayo.

Wafanyakazi wawili wa kutoa misaada wameliambia shirika la habari la Reuters kuwa kulikuwa na mapigano makali mpakani.

Haikuthibitisha kama wanajeshi wa Eritrea walikuwa wamevuka kuingia Tigray.Wiki iliyopita, BBC Tigrinya iliripoti kwamba Eritrea ilikuwa inawakusanya wanajeshi wa akiba ili kuimarisha jeshi lake.

Taarifa za uhamasishaji zilisambazwa katika mji mkuu wa Asmara, mji wa pili kwa ukubwa, Keren, mji wa magharibi wa Tessenai na maeneo mengine, mashuhuda walisema.

Hata hivyo, Waziri wa Habari wa Eritrea Yemane Gebremeskel alisema kuwa "idadi ndogo" ya askari wa akiba imeitwa, akikana kwamba watu wote walikuwa wamehamasishwa.

Chanzo: BBC