Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Eritrea imejiunga tena na Jumuiya ya Afrika Mashariki

Eritrea Imejiunga Tena Na Jumuiya Ya Afrika Mashariki Eritrea imejiunga tena na Jumuiya ya Afrika Mashariki

Tue, 13 Jun 2023 Chanzo: Voa

Eritrea ilianza tena shughuli zake katika IGAD na kuchukua kiti chake katika mkutano ulioandaliwa na jumuiya ya mataifa saba nchini Djibouti siku ya Jumatatu, Meskel alisema kwenye mtandao wa Twitter

Eritrea imejiunga tena na Jumuiya ya Afrika Mashariki, (IGAD), karibu miaka 16 baada ya taifa hilo lililojitenga kisiasa kujiondoa kutoka kwa chombo hicho, Waziri wa Habari wa Eritrea, Yemane Meskel alisema Jumatatu.

Eritrea ilianza tena shughuli zake katika IGAD na kuchukua kiti chake katika mkutano ulioandaliwa na jumuiya ya mataifa saba nchini Djibouti siku ya Jumatatu, Meskel alisema kwenye mtandao wa Twitter.

Alisema nchi hiyo iko tayari kufanya kazi kuelekea amani, utulivu, na ushirikiano wa kikanda.

Nchi hiyo ya kiimla ilisitisha uanachama wake wa IGAD mwaka 2007 kufuatia msururu wa kutoelewana, ikiwa ni pamoja na uamuzi wa Umoja huo kuitaka Kenya kusimamia utatuzi wa mzozo wa mpaka, kati ya Ethiopia na Eritrea.

Eritrea ilijitenga na Ethiopia mwaka 1993 na kupigana vita vya mpakani vya miaka miwili na jirani yake ambavyo vilitia sumu mahusiano pamoja na makubaliano ya amani mwaka 2018.

Kufuatia ushirikiano na Addis Ababa, wanajeshi wa Eritrea waliunga mkono vikosi vya Ethiopia wakati wa vita vya serikali kuu dhidi ya Tigray People's Liberation Front (TPLF) na wamekuwa wakishutumiwa na Marekani na makundi ya haki za binadamu, kwa baadhi ya vitendo vya ukatili mbaya zaidi wa vita.

Chanzo: Voa