Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Equatorial Guinea yathibitisha kuzuka kwa virusi vya Marburg

Equatorial Guinea Yathibitisha Kuzuka Kwa Virusi Vya Marburg Equatorial Guinea yathibitisha kuzuka kwa virusi vya Marburg

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: Bbc

Mamlaka nchini Equatorial Guinea siku ya Jumatatu ilisema nchi hiyo iliripoti mlipuko wake wa kwanza wa virusi vya Marburg, ugonjwa unaoambukiza sana katika familia moja ya virusi vinavyosababisha Ebola.

Watu tisa wanashukiwa kufariki kutokana na homa ya virusi hivyo katika mkoa wa magharibi wa Kie Ntem nchini humo.

Vipimo Zaidi vilivyofanywa kwenye sampuli moja ambayo ilikusanywa na kusafirishwa kwa Institut Pasteur huko Dakar, Senegal, vilipatikana kuwa chanya.

Shirika la Afya Ulimwenguni linasema watu 16 sasa wako chini ya karantini .Shirika la afya limetuma timu ya wataalam katika eneo hilo kusaidia wafanyikazi wa afya.

Wiki iliyopita, Waziri wa Afya wa nchi hiyo Mitoha Ondo'o Ayekaba alisema uchunguzi wa awali ulihusisha vifo hivyo na watu waliohudhuria hafla ya mazishi.

Huu ni mlipuko wa kwanza kuripotiwa nchini na wa tatu Afrika Magharibi. Ghana ilithibitisha kisa kimoja mwaka jana na Guinea mwaka uliotangulia.

Virusi hupitishwa kwa watu kutoka kwa popo wa matunda na huenea kati ya wanadamu kupitia upitishaji wa maji ya mwili.

Ingawa hakuna chanjo au matibabu, wale waliogunduliwa wanashauriwa kunywa maji mengi kwani madaktari hutibu dalili za ugonjwa.

Milipuko ya awali na visa vya hapa na pale vya Marburg barani Afrika vimeripotiwa nchini Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kenya, Afrika Kusini na Uganda.

Chanzo: Bbc