Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Equatoria Guinea: Mahakama yatoa hati ya kukamatwa Carmelo

Equtorial Guinea.png Equatoria Guinea: Mahakama yatoa hati ya kukamatwa Carmelo

Fri, 23 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama kuu nchini Uhispania, imekubali rufaa ya wanachama kadhaa wa upinzani nchini Equatoria Guinea, na kuagiza mahakama ya chini kutoa hati ya kukamatwa kwa mtoto wa rais wa nchi hiyo, Carmelo Ovono Obiang Nguema.

Carmelo na maafisa wengine wawili waandamizi walishtakiwa kwa kuwateka nyara wanachama wanne wa kundi la upinzani lenye makao yake nchini Uhispania, walipokuwa safarini kwenda Sudan Kusini mwaka 2019.

Awali mahakama hiyo ilitangaza kuwa imeanza kumchunguza tangu kutolewa kwa madai hayo, ambayo Wadadisi walisema huenda yakaharibu juhudi za rais huyo kuboresha sifa yake kimataifa.

Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ametawala koloni hilo la zamani la Uhispania lenye utajiri mkubwa wa mafuta tangu 1979, na amekuwa akijipatia ushindi kwenye chaguzi kadhaa za nchi hiyo, na sasa yuko madarakani kwa muhula wa sita

Chanzo: www.tanzaniaweb.live