Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Endeleza handisheki kwa DP Ruto, Kabogo amwambia Rais Uhuru

Cdb80cf8390f6668 Endeleza handisheki kwa DP Ruto, Kabogo amwambia Rais Uhuru

Mon, 21 Jun 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Kabogo alikumbusha Uhuru na Ruto kuhusu urafiki wao wa kuvaa shati zinazofanana na kuwataka kurudianaAlisema umoja wa taifa ni muhimu kwa hivyo viongozi wote wanafaa kumaliza uhasama wa kisiasaAlitaka eneo la Mt Kenya kuungana ili kuhakikisha 2022 wana sauti kubwa katika debeAliyekuwa gavana wa Kiambu William Kabogo amemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutafuta suluhu la tofauti zake na naibu wake William Ruto.

Kabogo alisema wawili hao wanafaa kumaliza uhasama wao ili umoja wa wafuasi wao ushuhudiwe kama ilivyokuwa kuanzia 2013.

"Ruto alinitembelea miezi kadhaa iliyopita na nikamwambia, nyinyi mlikuja kwetu mkiwa pamoja. Ni nini kimefanyika sasa kiasi kwamba hatuwaoni pamoja tena?" alisema Kabogo.

Alitaka Rais kuketi na kuhakikisha kuna handiseki yake na DP kama vile alivyofanya kwa kinara wa upinzani Raila Odinga.



"Taifa hili ni kuhimu kuliko yeyote kati yao. Tuwaombee ili handisheki ifikishwe kwa Ruto na kila kiongozi ili taifa hili liweze kusonga mbele," aliongeza Kabogo.

Mwanasiasa huyo wakati huo pia aliwatalka wakazi wa MT Kenya kuhakikisha wanasalia na umoja wao kisiasa ili kuwa na sauti nzito ifikapo 2022.

"Sisi tukae pamoja ili nani au nani akikuja atupate pamoja. Si muhimu tutakapoenda, lakini tuwe kitu kimoja. Tusipofanya hivyo, tutabebwa ufala," alisema.



Kenyatta na naibu wake wamekuwa na tofauti za kisiasa tangu Rais afanye handisheki na Raila Odinga.

Tayari sasa kilichokuwa chama chao cha Jubilee kimebaki mahame kwa wandani wa Ruto ambao sasa wanajihusisha na United Democratic Alliance (UDA).

Ruto kwa mara ya kwanza Jumamosi Juni 19 alisema anajipanga na gari lake la kuingia Ikulu 2022 sasa ni UDA.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka TUKO

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke