Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Emmanuelle Eboue, Kutoka mwanasoka milionea hadi kupanda `daladala’

0e82709fe8937e633f662ba8479f8304 Emmanuelle Eboue, Kutoka mwanasoka milionea hadi kupanda `daladala’

Mon, 8 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WACHEZAJI wa Afrika wanaocheza soka Ulaya hasa nchi kama Uingereza, Ufaransa, Ujerumani na Italia wengi wao wamekuwa wakipata fedha nyingi kutokana na mishahara au bonasi.

Wachezaji wawili wa Ivory Coast waliokuwa wakicheza soka katika Ligi Kuu ya England, Emmanuelle Eboue na Didier Drogba. Wachezaji wote klabu kubwa jijini London katika kipindi kimoja.

Ni karibu muongo mmoja wachezaji hao walicheza soka katika kiwango cha juu katika Ligi Kuu ya England wakati Drogba akiwa Chelsea mwenzake Eboue alikuwa akikipiga Arsenal.

Kila mchezaji Ivory Coast alikuwa akipata maelfu ya Pauni kwa wiki kwa wastani wa kipindi cha miaka nane. Hilo lina maana kuwa wachezaji hao walikuwa mabilionea baada ya kumaliza kipindi chao katika klabu hizo.

UTAJIRI MKUBWA

Lakini wakati Didier Drogba sasa ni tajiri mkubwa na sio tu mwekezaji wa pili katika madini huko kwao Ivory Coast (bila kutaja kuwa ni sehemu ya mmiliki wa klabu mbili za soka za MLS huko Amerika ya Kaskazini wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 100).

Lakini stori ya Eboue ni tofauti kabisa kwani yeye baada ya kuachana na mkewe mzungu, ambako jaji alimpatia mwanamke huyo mali pamoja na nyumba za mchezaji huyo, amebaki kuwa maskini wa kutupwa.

Mchezaji huyo alijikuta akiishi katika nyumba isiyo na hata umeme na sasa ana wakati mgumu na hana kitu.

Mchezaji huyo sasa anafua nguo zake kwa mikono badala ya kutumia mashine kama ilivyo kwa wachezaji na watu wengi Ulaya (na shukrani kwa bibi yake ambaye alimfundisha kazi za nyumbani wakati akikuwa kijijini), kwani imemsaidia kujipikia.

Kwa miaka mingi nje ya nyumba yake alikuwa akipaki magari ya kifahari, lakini sasa sio yeye tena kwani akitaka kwenda mjini au mahali kwingine amekuwa akitumia usafiri wa umma. Amekuwa akimlamu mkewe wa zamani kwa hali hiyo.

“Emmanuelle sasa hana kitu,” Eboue sasa amekuwa mchovu. “Kila dokumenti ambayo mke alikuambia kusaini, ulisaini bila hata ya kuangalia (hata iliyohusu mali)!” Alibainisha kuwa kati ya Euro milioni 8 alizopata wakati akiichezea Galatasary huko Uturuki, milioni saba zilitumwa kwa mke wake wazamani Aurelie.

Mke huyo alikuwa akitumia fedha hizo kwa sababu alikuwa akiishi na watoto watatu aliyezaa na mchezaji huyo jijini London. Kwa sasa mke huyo amekata mawasiliano ya baba na watoto hao.

Hapa kuna somo la kujifunza kutoka katika janga la Eboue (kwa kweli ni zaidi ya huzuni, kwa sababu utajiri wa mamilioni ya Pauni aliokuwa nao mchezaji huyo, sasa umekuwa katika janga kubwa.

NDOA YA DROGBA

Mwenzake Drogba mwenyewe alifunga ndoa na mwanamke wa Mali kama kuoa mwanamke mrembo wa Tanzania. Kikubwa ukioa mwafrika mwenzako mali nyingi zitarudi nchi kwako, ambako ndiko kwenye asili yako.

Endapo Eboue angejenga nyumba za kupangisha jijini Abidjan, bila shaka jaji Muingereza asingeweza kumzawadia Aurelie nyumba hizo.

Ukweli Drogba amewekeza sana huko Marseilles, pamoja na kujenga nyumba za kupangisha Ivory Coast alipowekeza sehemu ya madini wakati wa vita vya wentewe kwa wenyewe kwa bei nafuu.

Drogba pia ni mtu mwingine wa aina yake kwani amejenga hospitali kubwa kwa ajili ya watu maskani Ivory Coast jijini Abidjan, bado anaendelea kuwasiliana na tajiri mkubwa Abramovich.

“Kwa kutumia mawasiliano au kujuana na watu wenye uwezo na kutumia busara zake, Drogba sasa ni maarufu sana nchini Ivory Coast (Sawa na mwanasoka mkubwa nchini Liberia, George Weah).

Eboue aliwekeza vitu vya kijinga kwa mkewe huyo mzungu kama kununua magari ya kifahari na mambo mengine.

Wakati Eboue hajaenda shule, mwenzake Drogba ni mhasibu msomi (mwenye kiwango cha shahada), Eboue ana kipaji lakini hakijamsaidia.

Hatahivyo, Eboue kwa sasa anapitia maisha magumu sana na amemua kumrudia mchumba wake wa zamani aliyemtosa na kumuoa mzungu.

Nyota huyo wazamani wa Arsenal sasa ameamua kumrudia na kumuoa mpenzi wake wa zamani aliyemtosa.

Hivi karibuni nyota huyo wazamani wa Arsenal na Ivory Coast alifunga ndoa jijini Abidjan baada ya kuachana na mke wake wa kwanza aliyekuwa mzungu, Aurélie.

Kwa mujibu wa Mondialsport, mke huyo wa sasa wa Eboue alikuwa mchumba wake wa muda mrefu kabla mchezaji huyo hajahamia Ulaya na kumuoa mke wake huyo Mbelgiji aliyemfilisi.

Chanzo: habarileo.co.tz