Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Embu: Suti ya Mchungaji yawakosanisha washiriki kanisani

0fgjhs2q02vu4hj6jg Embu: Suti ya Mchungaji yawakosanisha washiriki kanisani

Sat, 10 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

Sinema ya bwerere ilitokea katika kanisa moja eneo la Machang’a, Embu wakati waumini walianza kubishana wakiwalaumu wenzao kwa kukosa kushiriki shughuli ya kuchanga pesa za kununulia pasta suti.

Duru zinaarifu kwamba baadhi ya washiriki wa kanisa walipendekeza pesa zichangwe ili pasta anunuliwe suti lakini wengine hawakuchangamkia mpango huo.

Kwa mujibu wa Taifa Leo, siku ya kioja mweka hazina w mpango huo aliudhika na jinsi baadhi ya washiriki walivyojitia hamnazo licha ya kufahamu kuwepo kwa mchango huo.

“Mtachanga pesa ama hamchangi? Tunagaa kuchanga KSh10,000za kumnunulia pasta wetu suti. Pasta anapaswa kuwa nadhifu kila wakati anapotuhubiria na akiwa katika shughuli za kueneza injili,” mweka hazina alisema.

Hata hivyo, fujo zilianza wakati sehemu moja ya waumini walipinga vikali na kuanza kurusha cheche za maneno.

“Kwa nini huwa mnapanga mambo yenu kiholela bila kutushirikisha na kusikia maoni yetu. Tukichanga pesa hizo tutakuwa tunaendelea shughuli ya ubinafsi na haina msingi wowote. Kwa nini tusichange pesa kwa miradi iliyo na manufaa kwa kila mtu katika kanisa hili?

“Baadhi ya waumini na watoto huwa wanavaa matambara, mbona hatuwafikirii. Tusipendelee mtu mmoja ilhali kuna wengi wanaofaa kusaidiwa,” muumini mmoja alisema.

Inasemekana matamshi ya muumini huyo yaliwaudhi mno washirika waliokuwa wanaunga mkono pendekezo hilo na nidposa mabishano makali yakazuka huku kila mmoja akitoa maoni yake.

Penyenye zinasema waliokuwa wakiunga mkono mchango huo walidai kutomfaa pasta ni kujinyima Baraka nao waliopinga nao wakidai mchungaji hakuwa akiwajali wumini waliohitaji msaada.

Maji yalipozidi unga, ilimbidi mmumini mmoja ambaye pia ni mzee wa kanisa kuingilia kati na kutuliza hali.

Wakati wa purukushani hiyo, inasemekana mtumishi wa Mungu alikuwa ameenda ziara ya dharura.

Hata hivyo, haijulikani alichukua hatua gani aliporejea na kufahamishwa kilichojiri.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke