Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Edgar Lungu apokonywa marupurupu ya kustaafu

Edgar Lungu: Rais Wa Zamani Wa Zambia Apokonywa Marupurupu Ya Kustaafu Edgar Lungu apokonywa marupurupu ya kustaafu

Thu, 2 Nov 2023 Chanzo: Bbc

Serikali ya Zambia imeondoa marupurupu ya kustaafu na mafao mengine kutoka kwa Rais wa zamani Edgar Lungu kufuatia uamuzi wake wa kurejea katika siasa.

Bw Lungu alipoteza urais baada ya kushindwa na Hakainde Hichilema mwaka wa 2021, na kisha akatangaza kustaafu.

Baada ya miaka sita madarakani aliacha nchi ikikabiliwa na matatizo mazito ya kiuchumi likiwa taifa lenye deni kubwa zaidi barani Afrika.

Kurejea kwake katika siasa kunamweka katika nafasi nyingine ya kuleta kinya’ng’anyiro kikali mazingira cha urais 2026.

Rais huyo wa zamani tayari amearifiwa kuhusu kuondolewa mara moja kwa marupurupu yake ya kustaafu, kulingana na msemaji wa serikali Cornelius Mweetwa.

Akiwa rais mstaafu, Bw Lungu alikuwa na haki ya kuwa na maafisa watatu wa usalama, pasipoti ya kidiplomasia, magari matatu ya serikali, nyumba yenye samani, bima ya matibabu na gharama za mazishi juu ya kifo chake.

Pia alikuwa na kinga dhidi ya kufunguliwa mashitaka. Katika kikao na wanahabari siku ya Jumatano, Bw Mweetwa alisema kiongozi huyo wa zamani sasa atashughulikiwa kwa "usawa wa sheria", sawa na raia mwingine yeyote mkuu nchini.

Chanzo: Bbc