Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ecowas yaamuru kuachiwa huru Rais wa Niger aliyepinduliwa

Niger Rais Mapunduziiiii Ecowas.jpeg Ecowas yaamuru kuachiwa huru Rais wa Niger aliyepinduliwa

Sat, 16 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) jana iliamuru kuachiliwa mara moja na bila masharti Rais aliyepinduliwa wa Niger Mohamed Bazoum.

Mahakama hiyo ya Ecowas jana iliamuru kurejeshwa kwa Bazoum, ambaye alipinduliwa mamlakani na jeshi Julai 26 mwaka huu ikisema kuwa bado ni Rais halali wa Niger. Mohamed Bazoum na familia yake wamekuwa kizuizini katika ikulu ya Rais wa Niger licha ya matakwa mbalimbali ya jumuiya ya Ecowas na nchi nyingine kwa ajili ya kumuachia huru rais huyo aliyepinduliwa wa Niger.

Itakumbukwa kuwa Bazoum mwezi Septemba mwaka huu aliwasilisha kesi katika mahakama ya Ecowas akihoji kuhusu kupinduliwa na jeshi, kutiwa nguvuni na kuwekwa kizuizni na viongozi wa kijeshi; ambapo alitaka kuachiwa huru na kurejeshwa mamlakani kama Rais wa Niger.

Aidha tarehe8 mwezi huu wa Disemba mahakama hiyo ya jumuiya ya Ecowas ilitupilia mbali kesi iliyokuwa imewasilishwa na utawala wa kijeshi wa Niger uliotaka kuondolewa nchi hiyo vikwazo vilivyowewa na viongozi na serikali za magharibi mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live