Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Earth is Hard: Wanamtandao Wamcheka Wakuraya Baada ya Kushindwa Kumpata Muthoni

D19b0ff8222bf137 Earth is Hard: Wanamtandao Wamcheka Wakuraya Baada ya Kushindwa Kumpata Muthoni

Mon, 12 Jul 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Wanamtandao walisema Ken Wakuraya aliishia kuchotea wageni maji katika harusi ya Muthoni wa Mukiri

- Wawili hao walisoma taarifa pamoja katika runinga ya Inooro na wengi kudhani kuwa wangeishia kuwa 'couple ya pawa'

- Muthoni alitekwa na dume mwingine na kufanya harusi ya kitamaduni ambapo kuraya aliburudisha wageni

Wanamtandao ni watu watani sana na wikendi wametumia weledi wao wa kuwavunja wengine mbavu kumtania mtangazaji Ken Wakuraya.

Ni wazi kuwa Wakuraya, ambaye ni maarufu kama msomaji wa habari runinga ya Inooro, amekuwa na wakati mgumu wikendi.

Masaibu ya mtangazaji huyo yalianza baada ya aliyekuwa msomaji wa habari mwenzake Muthoni wa Mukiri kufunga ndoa na barafu wake wa roho.

Muthoni alifanya harusi ya kitamanduni ambapo wazazi wake walimpeana na dume aliyeyeyusha roho yake.

Wakuraya naye aliitwa kwenye harusi hiyo kuwa burudisha wageni waliokuwa wamefika kushuhudia Muthoni akifunga ndoa.



Read also

Caroline Kangogo: DCI Yashindwa Kufuatilia Nyayo za Mshukiwa Baada ya Kuzima Simu

Kwa kuwa Muthoni na Wakuraya wamekuwa katika runinga ya Inooro kwa muda pamoja, wengi walikuwa wamewaona kama ‘couple ya pawa’.

Walifanya taarifa kwa pamoja kwa njia ya kuvutia kiwango kwamba wengi walihisi kulikuwa na ‘Chemistry’ kati yao na kufikiri Wakuraya angezheza kama yeye.



Mara kwa mara, Macho ya Wakuraya yalionekana yamejaa tamaa ya kuwa na uhusiano zaidi yaw a kazini na kipusa huyo.

Wengi walifananisha wawili hao na wenzao kwenye runinga ya Citizen Rashid Abdalla na Lulu Hassan ambo ni wapenzi wa kwanza kuwa katika runinga kusoma taarifa kwa wakati mmoja.

Lakini wapi! Wakuraya alishindwa kucheza kama yeye na kufanya dume mwingine kuitwaa dunia ya Muthoni.

Kwenye mtandao, ucheshi ulijaa huku Wakuraya akifananishwa na methali ya ‘If you hang around a beautiful gril without saying a word you will end up fetching water for guests at her wedding’.



Read also

Mmoja Akamatwa kwa Kutangaza Kifo cha Rais Yoweri Museveni

Sasa wanatmdao walipata methali mpya ya ‘If you stay around a beautiful girl without saying a word, you will end up entertaining guests at her wedding’.

Kutoka meza ya TUKO.co.ke, tunawataki Muthoni na dume wake kila la kheri maishanni, kwa Wakuraya ‘iza bro’.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 073248269.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka TUKO hapa

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke