Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EU yawezesha ukuaji wa viwanda vidogo vidogo nchini Botswana

EPA BOTSWANA.png EU yawezesha ukuaji wa viwanda vidogo vidogo nchini Botswana

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Ulaya kupitia mpango wake wa kiuchumi wa EPA na mataifa ya Kusini mwa Afrika SADC, umetenga Euro Milioni 6 kusaidia kuinua na kuanzisha viwanda vidogo vidogo na kuimarisha ujasiriamali.

Botswana ni miongoni mwa nchi zinazonufaika na mpango huo ambao, bajeti yake inatarajiwa kumalizika Julai 2024. EU inashirikiana na mamlaka ya uwekezaji wa ndani LEA, kuwatambua na kuwaendeleza wajasiriamali.

Msaada huo uweiwezesha mamlaka hiyo kuisaidia kutangaza bidhaa mbalimbali zinazozalishwa nchini na kuzitafutia soko nje ya nchi.

Shetho Orapeleng, Meneja anayehusika na upatikanaji wa masoko kutoka mamlaka hayo, anasema licha ya msaada wa EU, anasema changamoto kubwa inasalia kupata soko la Kimataifa. Nchi hiyo pia inauza nyama na ngozi pamoja na nguo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live