Wed, 26 Oct 2022
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Walioondolewa vikwazo ni Waziri Mkuu Gervais Ndirakobuca, Godefroid Bizimana Mshauri Mkuu wa Rais, na Leonard Ngendakumana, Afisa Mkuu wa zamani wa Jeshi.
EU imesema imeridhishwa na masuala ya Haki za Binadamu yanavyochukuliwa kwa uzito pamoja na mazungumzo yanayoendelea kati ya Serikali na Umoja huo.
Mwaka 2015, EU iliweka vikwazo vya kusafiri na kuzuia mali kwa maafisa kadhaa wa Burundi baada ya kuwashutumu kudhoofisha Demokrasia kabla ya uchaguzi wa marudio wakati wa utawala wa Hayati Pierre Nkurunziza.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live