Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EU yaombwa kusaidia kuondolewa vikwazo Sudan Kusini

17c5a58b468b18e977b6d64800852762 EU yaombwa kusaidia kuondolewa vikwazo Sudan Kusini

Tue, 16 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

SUDAN Kusini imeuomba Umoja wa Ulaya (EU) kusaidia kuondolewa vikwazo mbalimbali viliyowekwa na Marekani nchini.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Deng Dau Deng amesema wanaiomba EU kusaidia kuishawishi Marekani na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuondoa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya nchi hiyo tangu 2017.

Alisema vikwazo vya upande mmoja vilivyowekwa na Markani viliidhinishwa na EU na ndio maaba serikali inatafuta msaada wa umoja huo.

"Tuna wasiwasi sana kuhusu maofisa wetu wa serikali ambao wamewekewa vikwazo na UN na Marekani," alisema na kuongeza kuwa kwa sasa wanatekeleza mkataba wa amani hivyo hakuna sababu ya kubakia vikwazo.

Mwaka 2017 Marekani iliweka vikwazo kwa maofisa wakuu wa Sudan Kusini wakiwemo wa wa jeshi, kwa madai kuwa wanazuia mchakato wa amani.

Serikali ya Sudan Kusini imesema vikwazo vya silaha vinakatisha tamaa juhudi za serikali kutekeleza makubaliano ya amani,

Deng alisema UNSC Julai, 2018 iliweka vizuizi vya silaha kwa Sudan Kusini kufuatia ghasia zilizozuka Julai, 2016 ambazo zilivunja makubaliano ya amani ya 2015 yaliyotiwa saini kumaliza mzozo wa miaka mingi nchini.

Maofisa waliowekewa vikwazo ni pamoja na Makamu wa Rais, Taban Deng Gai, Mshauri wa Rais, Kuol Manyang Juuk, Waziri wa Masuala ya Baraza la Mawaziri, Martin Elia Lomuro na Waziri wa Habari, Michael Makuei.

Chanzo: habarileo.co.tz