Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EU yakosa la kufanya mapinduzi Gabon

Maafisa Wa Jeshi Wasema Wamechukua Mamlaka Gabon EU yakosa la kufanya mapinduzi Gabon

Fri, 1 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema kwamba umoja huo hauna mpango wa kuwaondoa wafanyakazi wake nchini Gabon kwa sababu hali nchini humo ni shwari.

Kwa mujibu wa shirika la habari la IRNA; Burrell amesema hayo kabla ya mkutano usio rasmi wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya uliofanyika Toledo, Uhispania, na kuongeza kuwa: "Tunafuatilia kwa makini matukio ya hivi karibuni katika nchi hiyo ya Afrika ya Kati, lakini kwa sasa hatuoni umuhimu wa kuwahamisha wajumbe wetu kutoka Gabon, tofauti na tulivyofanya nchini Niger kwa sababu hali nchini Gabon hivi sasa ni shwari na hakuna vurugu."

Jumatano ya juzi, maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi wa Gabon waliipindua serikali ya makumi ya miaka ya ukoo wa Bongo na walitangaza kubatilisha matokeo ya uchaguzi yaliyomrejesha madarani rais wa muda mrefu, Ali Bongo. Josep Borrell

Mkuu wa Sera za Kigeni za Umoja wa Ulaya amesisitiza kuwa mapinduzi ya kijeshi si suluhisho sahihi, hata kama kulikuwa na dosari katika upigaji kura wa siku ya Jumamosi na kwamba Umoja wa Ulaya utaendelea na juhudi zake za kidiplomasia za kukabiliana na matukio ya hivi karibuni ya nchini Gabon.

Baada ya mapinduzi ya kijeshi ya juzi Jumatano, serikali ya kijeshi ya Gabon ilimtangaza Jenerali Brice Oligui Nguema kuwa mkuu wa serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Rais aliyeondolewa madarakani wa Gabon, Ali Bongo, sasa yuko chini ya kizuizi cha nyumbani, na mmoja wa wanawe wa kiumbe amekamatwa kwa tuhuma za uhaini.

Ali Bongo Ondimba alikuwa rais wa Gabon kwa mara ya kwanza mnamo 2009. Alitangazwa mshindi wa uchaguzi mkuu wa siku ya Jumamosi kwa muhula mtatu mfululizo ambapo tume ya uchaguzi wa Gabon ilitangaza kuwa Ali Bongo amepata ushindi wa asilimia 64.27 ya kura.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live