Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EU sasa kuiondolea  vikwazo Burundi

7e81083e0b9285e8bfafe4b3d5e2dcfe.png EU sasa kuiondolea  vikwazo Burundi

Tue, 29 Jun 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

UMOJA wa Ulaya (EU) umeanza mchakato wa kuondoa vikwazo kwa Burundi.

Umoja huo uliiwekea Burundi vikwazo mwaka 2015 wakati wa machafuko ya kisiasa baada ya Rais wa zamani, Rais Pierre Nkurunziza kuongeza muda wa kuongoza na kusababisha maandamano.

Balozi wa EU nchini Burundi, Claude Bochu aliwaambia waandishi wa habari juzi kuwa, mwisho wa Mei mwaka huu, vikosi kazi vya EU viliamua kwa kauli moja taasisi za Mahakama za umoja huo kubatilisha kusimamishwa kwa msaada wa kifedha kwa serikali ya Burundi.

Alisema hatua hiyo ilifikiwa baada ya kufanya mkutano na Rais wa Burundi, Evariste Ndayishimiye na kuona maendeleo makubwa chini ya utawala wake katika kukuza utawala wa sheria na haki za binadamu.

Alisema EU inatarajia matokeo mazuri zaidi na kuwa pamoja na washirika wengine kama Benki ya Maendeleo ya Afrika watagharamia ukarabati wa Bandari ya Bujumbura na maeneo yake ya karibu kabla ya mwisho wa mwaka huu na kuchangia fedha katika sekta ya kilimo.

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) hivi karibuni ilitoa mwito kwa EU kuondoa vikwazo kwa Burundi, ikisema nchi hiyo iko tayari kusonga mbele.

Katibu Mkuu wa EAC, Peter Mathuki alisema vikwazo hivyo vinawaumiza wananchi wa Burundi pamoja na watu wote wa ukanda wa Afrika Mashariki.

EAC inajumuisha nchi sita za Burundi, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Sudan Kusini.

Chanzo: www.habarileo.co.tz