Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EU kutotuma wasimamizi wa uchaguzi mkuu Uganda

Ac07911553ddf4404c96b1cee524b8d0 EU kutotuma wasimamizi wa uchaguzi mkuu Uganda

Tue, 22 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

UMOJA wa Ulaya (EU) umesema hautatuma waangalizi wake kufuatilia uchaguzi mkuu wa Uganda kwa sababu mapendekezo yake baada ya uchaguzi wa mwaka 2016 hayakutiliwa maanani na serikali.

Taarifa iliyotolewa na umoja huo mwishoni mwa wiki ilisema umeamua kutotuma waangalizi wake kwa sababu kuna kila dalili za kutofanyiwa kazi mapendekezo yao kama ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita.

Kwa kawaida Umoja wa Ulaya hutuma idadi kubwa ya waangalizi katika uchaguzi mbali mbali barani Afrika na sehemu nyingine duniani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Umoja wa Ulaya ya mwaka 2018 serikali ya Uganda haikutilia maanani mapendekezo yake yote 30 ya mwaka 2016 juu ya namna ya kuandaa uchaguzi ulio huru na haki.

Ripoti hiyo imesema hakuna pendekezo lolote limetekelezwa wala serikali kuonesha nia ya kutaka kutekeleza.

Miongoni mwa mapendekezo hayo ni kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, polisi na maofisa wa usalama kuacha kutumia nguvu dhidi ya wagombea wa upinzani na kuweka mazingira ya uwazi wakati kura zinahesabiwa.

Chanzo: habarileo.co.tz