Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EU imetoa msaada wa Dola za Marekani bilioni 8 kwa nchi ya Misri

EU Msaada.png EU imetoa msaada wa Dola za Marekani bilioni 8 kwa nchi ya Misri

Mon, 18 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Umoja wa Ulaya, umetangaza kuipa Misri kiasi cha dola za Marekani bilioni 8 kama mkopo na msaada, fedha inazotoa wakati huu nchi wanachama zikijaribu kukabiliana na wimbi la wahamiaji.

Mpango huo umetajwa kuwa unaboresha zaidi uhusiano wa EU na Misri.

Misaada, mikopo na fedha zingine zinapaswa kuwasilishwa katika kipindi cha miaka mitatu ijayo kusaidia uchumi unaodorora wa Misri.

Mgogoro wa kifedha unaoendelea kushuhudiwa nchini humo umesababisha kuongezeka kwa idadi ya raia wa Misri wanaojaribu kuvuka kuelekea Ulaya, hasa kupitia Libya kutafuta maisha bora.

Ursula von der Leyen ni rais wa Kamisheni ya umoja wa Ulaya.

“Nguzo ya nne ni uhamiaji na uhamaji ambapo tayari tuna ushirikiano mzuri sana na hii inahitajika zaidi kuliko hapo awali.” alisema Ursula von der Leyen ni rais wa Kamisheni ya umoja wa Ulaya.

Aidha EU imetangaza kutoa msaada zaidi kwa nchi hiyo kusaidia katika sekta ya nishati na ujenzi wa uchumi wake.

Misri ilijitolea kuzuia uhamiaji usio wa kawaida kwenda Ulaya.

EU katika siku za nyuma ilitia saini mikataba sawa na nchi nyingine za bara Afrika ambazo zinatumika kama njia kwa uhamiaji usio wa kawaida kwenda Ulaya, ikiwa ni pamoja na Tunisia, Libya na Mauritania.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live