Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECOWAS yaweka vikwazo Niger

Kamandi Ya Kijeshi Ya Niger Yatangaza Kuunga Mkono Mapinduzi ECOWAS yaweka vikwazo Niger

Mon, 31 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imelaani vikali mapinduzi ya kijeshi ya siku ya Jumatano nchini Niger ambayo yamemuondoa madarakani Rais Mohamed Bazoum. Wakati huo huo Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS nayo imetoa taarifa rasmi na kusema kwamba imeamua kuwawekea vikwazo majenerali wa kijeshi waliofanya mapinduzi dhidi ya rais aliyechaguliwa kidemokrasia huko Niger.

Makao Makuu ya OIC yako mjini Jeddah, Saudi Arabia. Shirika la habari la nchi hiyo limemnukuu Katibu Mkuu wa OIC Hissein Brahim Taha akisema kuwa, anafuatilia kwa wasiwasi mkubwa matukio ya nchi ya Niger ambayo ni mwanachama wa OIC.

Katibu Mkuu huyo wa OIC amelaani jaribio lolote la kunyakua madaraka kwa nguvu na kutaka Rais Bazoum aachiliwe huru mara moja na kurejeshwa utawala wa sheria nchini humo.

Hissein Taha ametilia mkazo msimamo wake wa kushikamana na wananchi wa Niger na uungaji mkono kamili wa OIC kwa juhudi za kikanda za kurejesha amani, usalama na utulivu katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, pamoja na eneo zima la Sahel. Rais Mohamed Bazoum wa Niger aliyepinduliwa na wanajeshi

Jumatano iliyopita, wanajeshi nchini Niger walimpindua Bazoum, rais aliyechaguliwa kidemokrasia. Vikosi vya Ulinzi na Usalama vya nchi hiyo vilisema katika taarifa yao kwa vyombo vya habari kupitia televisheni ya taifa siku ya Jumatano yaani saa chache baada za mapinduzi hayo kuwa rais huyo anashikiliwa na maafisa wa kijeshi waliofanya mapinduzi.

Wakati huo huo wakuu wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS, walitangaza jana Jumapili kuwa wameamua kuwawekea vikwazo maafisa wa kijeshi waliofanya mapinduzi huko Niger. Wakuu wa jumuiya hiyo ya kikanda ya nchi 15 wanachama, walikubaliana kuwawekea vikwazo viongozi wa kijeshi wa Niger waliohusika katika mapinduzi ya Jumatano iliyopita katika mkutano wa dharura uliofanyika jana Jumapili mjini Abuja, Nigeria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live