Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECOWAS yawataka wanasiasa wa Senegal waepuke vurugu

Ecowas Senegal ECOWAS yawataka wanasiasa wa Senegal waepuke vurugu

Wed, 7 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imewataka wanasiasa wa Senegal kujiepusha na ghasia na vitendo vingine vinavyoweza kudhoofisha amani na utulivu, baada ya tangazo la kuahirishwa kwa uchaguzi wa rais kuibua maandamano nchini humo.

Katika taarifa, ECOWAS imesema inafuatilia hali hiyo kwa wasiwasi na hivyo imewakumbusha wanasiasa jukumu lao katika kudumisha amani na utulivu katika nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika.

Siku ya Jumatatu, Bunge la Kitaifa la Senegal liliunga mkono muswada wa kuahirisha uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Februari 25 hadi Desemba 15. Wakati wa kikao hicho cha bunge, wabunge wa upinzani waliondolewa kwa nguvu kutoka ukumbini.

Maandamano yanayoongozwa na vyama vya siasa vya upinzani na baadhi ya mashirika ya kiraia yalizuka kote nchini humo siku ya Jumapili, siku moja baada ya Rais Macky Sally kutangaza kusimamisha uchaguzi wa urais kwa muda usiojulikana, akisema hatua hiyo imechukuliwa kutokana na mizozo kuhusu orodha ya wagombea na madai ya ufisadi wa majaji wa kikatiba. Rais Macky Sally wa Senegal

Karim Wade, mwana wa kiume wa rais wa zamani wa Senegal, na mpinzani mashuhuri wa serikali ya sasa ya Senegal, Ousmane Sonko ni miongoni mwa shakhsia walioondolewa kwenye orodha hiyo ya wagombea wa kiti cha urais.

Siku ya Jumatatu, waandamanaji nje ya Bunge la Kitaifa walitawanywa na polisi wa kutuliza ghasia mjini Dakar wakati wabunge walipokutana kwa ajili ya kura hiyo muhimu.

Polisi pia walitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji katika maeneo tofauti nchini siku ya Jumanne.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live