Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECOWAS yaongeza vikwazo vikali kwa Mali na Guinea

Edcowas Pic Mali ECOWAS yaongeza vikwazo vikali kwa Mali na Guinea

Mon, 8 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Kanda ya Afrika Magharibi, ECOWAS imeendelea kushikiria msimamo wa kutozirejesha nchi za Mali na Guinea zinazotawaliwa kijeshi katika umoja huo huku ikiweka vikwazo vipya na kushinikiza kurejeshwa kwa demokrasia.

Jumuiya hiyo imesema kuwa imefikia uamuzi wa kuweka vikwazo hivyo ambavyo vitazuia safari kwa nchi hizo za kuingia na kutoka kufuatia kuchelewesha kwa utawala wa kiraia katika mataifa hayo.

Nae Rais wa Tume ya uchuguzi ECOWAS, Jean-Claude Kasssi Brou, amesema kuwa hatua hiyo inakuja wakati wakiwa wanaandaa mchakato wa uchaguzi nchini Mali uliokuwa unatarajiwa kufanyika Februari 27, 2022.

Aidha ameongeza kusema kuwa nchi ya Mali imeshatuma ujumbe kwa Rais wa Ghana, Nana Akufo Addo anayeongoza jumuiya hiyo kumjulisha kuwa hawataweza kufanya uchaguzi kama ilivyokuwa imepangwa hapo awali.

"Hatua hii inazihusu serikali zote za mpito na siku si nyingi vikwazo hivi vitaanza kufanya kazi" Amesema Rais huyo wa Tume.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live