Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECOWAS yaitambua rasmi serikali ya Niger

ECOWAS Inakabiliwa Na Mtihani Mgumu Ukanda Wa Afrika Magharibi ECOWAS yaitambua rasmi serikali ya Niger

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi ECOWAS imeitambua rasmi serikali mpya ya Niger ikiwa ni katika kulegeza misimamo yake ya kisiasa na kiuchumi kuhusiana na nchi hiyo.

Omar Alieu Touray Mkuu wa Tume ya ECOWAS, amesema katika mkutano wa jumuiya hiyo huko Abuja, mji mkuu wa Nigeria kwamba timu ya wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo wanafanya mazungumzo na serikali ya kijeshi ya Niger ili kukabidhi madaraka katika kipindi kifupi. Wananchi wa Niger wanaunga mkono serikali ya kijeshi ya nchi hiyo

Wakuu wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi walikata uhusiano wao na Niger muda mfupi baada ya kuingia madarakani jeshi na hata kutishia kuingilia kijeshi ili kumrejesha madarakani rais aliyeng'olewa madarakani wa nchi hiyo Muhammad Bazum.

Mnamo Julai 26, 2023, walinzi wa rais wa Niger walifanya mapinduzi dhidi ya rais wa wakati huo, Mohamed Bazoum, na kumchagua Abdelrahman Tiani mkuu wa walinzi wa rais, kuwa mkuu wa baraza la mpito.

Baraza la Kijeshi la Niger lilichukua madaraka katika nchi hiyo huku likitaka kuondoka vikosi vya kigeni hasa vya Ufaransa huko Niger na kukomeshwa uingiliaji wa Paris katika masuala ya nchi hiyo. Msimamo huo ulipelekea utawala wa kijeshi kupata uungaji mkono mkubwa wa wananchi. Ndani ya Niger, mamia ya wafuasi wa baraza la kijeshi waliandamana mbele ya ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu, Niamey. Walimchukulia Bazem kuwa mwitifaki wa nchi za Magharibi hasa Ufaransa na huku wakiunga mkono kuondolewa kwake madarakani, walitaka Wamagharibi wasitishe uingiliaji katika mambo ya ndani ya nchi yao. Kiongozi wa kijeshi wa Niger

Serikali ya kijeshi ya Niger imetangaza rasmi kuwa haitarudi nyuma, kupatana na wasaliti na kuwa itawashinda maadui wa nchi hiyo.

Kwa upande mwingine, washirika wa kigeni na wa kikanda wa Niger walishawishiwa na Ufaransa kuzidisha mashinikizo dhidi yake. ECOWAS ni moja ya taasisi za kikanda ambazo sio tu zilikata uhusiano wote wa kisiasa na kiuchumi na Niger, bali pia ilitishia kuishambulia kijeshi nchi hiyo ikiwa Bazoum hangerejea madarakani. Kwa upande mwingine, serikali mpya ya Niger kwa kushirikiana na nchi za Burkina Faso na Mali ilitangaza kwamba haitakubaliana na uingiliaji wowote wa kigeni.

Hvi sasa, na baada ya miezi michache tokea kuchukua uongozi serikali mpya nchini Niger, ECOWAS imetangaza kuwa itaboresha uhusiano wake na nchi hiyo. Kwa hakika, kusimama imara viongozi wa sasa wa Niger, ambao wanaungwa mkono dhidi ya ukoloni wa Ufaransa, kumepelekea kushindwa hatua za uingiliaji wa kigeni katika nchi hiyo.

Niger ni moja ya nchi muhimu na zenye ushawishi mkubwa katika eneo la Afrika Magharibi, ambayo, kama zilivyo nchi nyingi za bara hilo, ina maliasili nyingi, hasa urani, almasi, dhahabu na makaa ya mawe. Pia inachukuliwa kuwa muhimu kwa mtazamo wa kisiasa na kijiografia.

Ni kutokana na sababu hiyo, ndipo nchi wanachama wa ECOWAS zikafadhilisha kuchangua njia ya maingiliano na mazungumzo na nchi hiyo badala ya kuitenga katika eneo hilo. Hasa, tukizingatia ukweli kwamba Niger inaungwa mkono na nchi nyingine mbili muhimu katika eneo hilo, ambazo ni Burkina Faso na Mali, na kuendelea kwa mzozo wa kisiasa kuhusu aina ya serikali Niger, kunaweza kuacha taathira mbaya katika eneo zima la magharibi mwa Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live