Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECOWAS yaiondolea vikwazo Niger

ECOWAS Yaiondolea Vikwazo Niger ECOWAS yaiondolea vikwazo Niger

Sun, 25 Feb 2024 Chanzo: Bbc

Jumuiya ya kanda ya Afrika Magharibi (ECOWAS) imetangaza kuondolewa kwa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Niger.

Hayo yalifikiwa katika mkutano wa viongozi mjini Abuja, wakitaka kupitisha mkakati mpya wa kuzishawishi nchi zinazoongozwa na wanajeshi kusalia katika umoja huo.

Vikwazo vya awali vililenga shughuli za usafiri, biashara na uchumi nchini kwa lengo la kugeuza mapinduzi ya Julai 26 ya mwaka jana na baadhi ya maafisa wa kijeshi.

Rais wa Tume ya ECOWAS Omar Alieu Touray ambaye alisoma maamuzi yaliyofikiwa na viongozi wa ECOWAS, alisema kuwa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Niger ni "kwa misingi ya kibinadamu" ili kupunguza mateso yaliyosababishwa na matokeo yake.

Viongozi wa kijeshi wa majirani watatu wa Sahel pamoja na Guinea sasa wako huru kushiriki katika masuala ya kiufundi na usalama ya umoja huo.

ECOWAS pia imetoa wito wa kuachiwa huru kwa rais aliyeondolewa madarakani Mohamed Bazoum, na kuzitaka nchi hizo nne kuwasilisha ratiba zao za mpito wa kidemokrasia.

Chanzo: Bbc