Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECOWAS ya ishtumu Serikali ya mpito Mali kwa kuchelewesha Uchaguzi Mkuu

Mali Ttt ECOWAS ya ishutumu Serikali ya mpito nchini Mali

Wed, 8 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya kikanda ya nchi za Magharibi ECOWAS, inaituhumu Seriklai yampito ya nchini mali kwa kutoa andaa mchakato wa uchaguzi kama walivyoahidi mapema mwezi Februari mwaka 2021.

Mapinduzi ya utawala wa nchini mali yaliyafanyika mwaka 2020 kwa kumuondoa Rais Ibrahim Boubacar Keita, jambo ambalo bado linatazamwa kwa ukaribu na Jumuiya hiyo kufuatia kukithiri kwa matukio ya mapinduzi ya kijeshi katikia ukanda huo wa magharibi mwa Afrika.

Awali uchaguzi huo ulipaswa kufanyika ndani ya mwezi February kabla ya kupigwa kalenda kwa madai ya marekebisho ya katiba, ambapo mwezi Mei Kiongozi wa Jeshi la mapinduzi nchini humo aliagiza kukamatwa kwa aliyekuwa Rais wa mpito wa nchi hiyo na kuchukua madaraka hayo yeye mwenyewe.

Hata hivyo mipango ya uchaguzi ilikuwa pale pale licha ya kugubikwa na sintofahamu nyingi kuhusu tarehe husika ya uchaguzi huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live