Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) inakabiliwa na changamoto kubwa kufuatia mlolongo wa mapinduzi katika nchi wanachama wa jumuiya hiyo.
Msururu wa mapinduzi katika ukanda wa Afrika Magharibi umeuweka umoja na uwezo wa jumuiya ya kikanda ya ECOWAS, katika mtihani, huku ikijaribu kurejesha utawala wa kiraia katika mataifa kama vile Burkina Faso, Guinea, Mali na Niger.
Mataifa hayo manne yameungana kupinga vikwazo vya kiuchumi, na hatua zinazoweza kuchukuliwa za kijeshi, na nchi zingine 11 wanachama wa jumuiya hiyo.
Weledi wa mambo wanaonya uwezo wa Jumuiya ya Kiuchumi ya mataifa ya Magharibi (ECOWAS) kushughulikia changamoto za kiusalama unahatarishwa na kuongezeka kwa viongozi wapya wa kijeshi miongoni mwa nchi wanachama. Majenerali wa kijeshi wa baadhi ya nchi wanachama wa ECOWAS
Jumuiya hiyo ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi inatatizika jinsi ya kukabiliana na utawala wa kijeshi nchini Niger, ambao umekuwa madarakani kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Mnamo Julai 26, wanajeshi walimweka Rais Mohamed Bazoum katika kizuizi cha nyumbani, wakishutumu utawala wake kwa kusimamia vibaya rasilimali za nchi na kuruhusu hali ya usalama kuzorota. Kwa kujibu, ECOWAS iliiwekea Niger vikwazo vya kibiashara na hata kutishia kuingilia kijeshi.
Lakini mizozo ya kisiasa na kiusalama inayoendelea nchini Niger, Burkina Faso, Guinea, na Mali inaonekana kuwa changamoto kwa nchi nyingine 11 wanachama wa ECOWAS.