Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECOWAS: Tuko tayari kufanya mazungumzo na nchi zilizojitoa

Ecowas Ecowasssssss ECOWAS : Tuko tayari kufanya mazungumzo na nchi zilizojitoa

Tue, 30 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika, ECOWAS, imesema iko tayari kufanya suluhu na nchi tatu zilizotangaza kujiondoa kwenye kambi hiyo kubwa ya Magharibi mwa Afrika.

Ni baada ya uamuzi uliochukuliwa na Wakuu wa Nchi za Mali, Niger na Burkina Faso wa kujiondoa kwenye taasisi hiyo muhimu ya kiuchumi ya kikanda, suala ambalo limepongezwa na raia katika eneo hilo.

ECOWAS imetangaza kuwa nchi hizo tatu zilikuwa wanachama muhimu kwenye jumuiya hiyo na kwamba imejitolea kutafuta suluhisho ya kisiasa kutatau mzozo kati yake na nchi hizo.

Viongozi wa nchi tatu za Mali, Niger na Burkina Faso zinazoongozwa na watawala wa kijeshi wameishutumu jumuiya hiyo ya kikanda ya Afrika Magharibi kuwa inashirikiana na mataifa makubwa kuzivuruga nchi zao. Vilevile wanalaumu vikwazo haramu, vya kinyama na visivyo halali vilivyowekwa dhidi ya nchi zao, ambavyo vinadhoofisha maisha ya raia wa kawaida.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya Nje wa Sierra Leone, Timothy Musa Kabba, amesema kuwa amesikitishwa na hatua hiyo na kuongeza kuwa ECOWAS hainshinikizwi na nchi za kigeni bali lengo lake ni kuhakikisha usalama na utulivuu wa kikanda.

Mataifa hayo matatu yamejitolea kujenga kambi mpya ya ushirikiano badala ya ile ya kiuchumi ya ECOWAS.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live