Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ECCAS yasimamisha uanachama wa Gabon

Kiongozi Wa Mapinduzi Ya Niger Jenerali Tchiani Aahidi Kukabidhi Madaraka ECCAS yasimamisha uanachama wa Gabon

Tue, 5 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia mapinduzi ya kijeshi nchini Gabon na kuondolewa madarakani rais wa nchi hiyo, baada ya Umoja wa Afrika kuchukua hatua, Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS) nayo imesimamisha uanachama wa nchi hiyo.

Tarehe 30 Agosti kundi la wanajeshi wa ngazi za juu nchini Gabon lilitangaza kufutwa matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika nchini, kuvunja taasisi zote za dola, na kusimamisha shughuli zote za serikali baada ya kumuondoa madarakani rais wa nchi hiyo na kuchukua madaraka.

Jeshi la Gabon limemtangaza Brice Oligui Nguema, ambaye hapo awali alikuwa kamanda wa kikosi cha ulinzi wa rais, kuwa mkuu wa serikali ya mpito.

Siku ya Jumatatu, ECCAS iliamua kusimamisha uanachama wa Gabon katika jumuiya hiyo na kutangaza kuwa uanachama wake utarejeshwa tu pale watawala wa nchi hiyo watakapokubali kurejeshwa nchini mfumo wa katiba.

ECCAS imelaani matumizi ya nguvu katika kutwaa mamlaka na kutatua mizozo nchini Gabon.

Baraza la Masuala ya Kisiasa, Amani na Usalama la Umoja wa Afrika lilitoa taarifa siku ya Alhamisi, likisimamisha ushiriki wa Gabon katika shughuli, vyombo na taasisi zake zote hadi pale utawala wa sheria utakaporejeshwa nchini.

Mapinduzi ya kijeshi nchini Gabon ni ya nane katika maeneo ya magharibi na katikati mwa bara la Afrika tangu mwaka 2020. Mapinduzi kama hayo yalishuhudiwa karibuni nchini Niger, ambayo yalifanyika Julai 26.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live