Mapambano dhidi ya umaskini, maendeleo endelevu na ushirikiano katika uchumi wa dunia wa nchi zinazounda Umoja wa Mataifa ya Afrika, Karibiani na Pasifiki yanabakia kuwa malengo makuu ya mkutano wa unaotarajia kufanyika nchini Angola, ambayo sasa inachukua nafasi ya mzunguko na urais wa EACP kwa miaka mitatu ijayo.
Ahadi hiyo, inayotokana na siku hii ya tatu ya mikutano tangulizi ya Mkutano wa 10 wa Wakuu wa Nchi na Serikali ulioanza hii leo Desemba 9, 2022 jijini Luanda, ambapo mkutano huo unafanyika kwa uwazi na ukiwa na umuhimu kwa vijana na wanawake wa Afrika ya baadaye.
Naibu katibu mtendaji wa SADC wa ushirikiano wa awali, Angèle Makombo na Katibu Mkuu wa EACP, Georges Chikoti wanasema wakuu wa nchi wanachama wanatarajiwa kujitolea mawazo yao kuona ni namna gani wataimarisha mshikamano ili kufikia lengo kusudiwa.
Mkutano huo unatarajia kumalizika hapo kesho Jumamosi Desemba 10, 2022 na kazi ya umaliziaji wa kusainiwa kwa Azimio la Luanda kwa ahadi hizo kuwekewa saini utatekelezwa na tayari Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasili nchini humo.