Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EAC yazindua mpango

5c02855fddb731b518d14c78ffa1367c EAC yazindua mpango

Tue, 13 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Na Theopista Nsanzugwanko

BALOZI wa EU nchini Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, Manfredo Fanti na Katibu Mkuu wa EAC, Libérat Mfumukeko, wamezindua mpango mpya wa Takribani Shilingi bilioni 43.87 kuimarisha ujumuishaji wa uchumi wa kikanda kupitia kuendeleza utekelezaji wa Umoja wa Forodha na Itifaki ya Soko la Pamoja.

Hasa, Malengo ya Ujumuishaji wa uchumi wa Kikanda (CORE) yatasaidia sana kuelekea Umoja wa Forodha kwa kusaidia itifaki ya habari, mawasiliano na teknolojia (ICT) katika ubadilishaji wa data katika usafirishaji wa bidhaa.

Programu ya CORE itasaidia utekelezaji wa utoaji huduma kwa kuruhusu kampuni kutoa huduma zao zaidi ya mipaka yao ya kitaifa na katika miaka miwili ya kwanza, lengo la programu hii litakuwa kwenye sekta za bima, uhasibu na usambazaji huku sekta nyingine zikifikiwa hao baadaye .

Kutokana na matumizi ya kidigitali , shughuli za forodha zitakuwa rahisi na salama wakati wa janga hil na hivyo kusababisha kupunguzwa kwa gharama za biashara ya mpakani.

Uwezo wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki utaimarishwa ili kuhakikisha kuwa taasisi hiyo inaweza kutekeleza agizo lake .

“Ushirikiano wa kiuchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ni msingi wa ajenda yetu ya ushirikiano. Mpango huu utakuwa kichocheo cha kufanya ujumuishaji wa uchumi kuwa wa kweli, "alisema Balozi Fanti.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa EAC ,balozi Mfumukeko alishukuru Jumuiya kwa msaada endelevu kutoka Jumuiya ya Ulaya kwenda EAC. Alisema makubaliano ya kifedha ufadhili yanakuja wakati muafaka wakati Jumuiya ikiazimisha Maadhimisho ya miaka 20, na kuongeza kuwa EU ilitoa mchango mkubwa kwa mafanikio yaliyofanywa na EAC katika nguzo zote nne za ujumuishaji, ambazo ni: Umoja wa Forodha, Soko la pamoja , Umoja wa Fedha na Shirikisho la Kisiasa.

“ni matumaini yangu kuwa ushirikiano wa EAC na EU utaimarika zaidi kutokana na kuwemo wa malengo ya amoja ya msingi,EU kwa miaka mingi wamekuwa watitupa misaada katika program mbalimbali za EAC katika amani na usalama,kukuza demokrasi n,utawala bora na uvuvi”alisema Mfumukeko.

Chanzo: habarileo.co.tz