Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EAC yashukuru kuunganisha vipaumbele vya uwekezaji

9cd95f07ad99670dac6296182dd01167 EAC yashukuru kuunganisha vipaumbele vya uwekezaji

Wed, 21 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki anayesimamia Sekta za Uzalishaji na Jamii, Christophe Bazivamo amewashukuru wataalamu wa Sekta ya Afya kwa juhudi za kutatua changamoto mbalimbali na kutoa mapendekezo na ushauri wa kitaalamu kwa ngazi za maamuzi ambayo yamepelekea utekelezaji wa mipango ya ubunifu katika hiyo na kuunganisha vipaumbele vya uwekezaji.

Bazivamo ametoa shukrani hizo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kawaida wa 20 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya ambao umeendelea leo kwa siku ya tatu katika Makao Makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.

Mkutano huo ulioanza Aprili 19,2020 ambao utafanyika kwa siku tano una lengo la kufanya mapitio ya hatua ya maendeleo iliyofikiwa katika utekelezaji wa maamuzi na maagizo yaliyotolewa na mkutano uliopita wa baraza hilo

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Leonard Subi amesema kuwa Tanzania imeendelea kuongeza mikakati ya kuzuia na kudhibiti janga la Covid-19.

“Tanzania tunadhamini juhudi zinazofanywa na Wanasayansi mbalimbali ulimwenguni katika kupata suluhisho la kudhibiti ugonjwa huu ikiwa ni pamoja na mshikamano ulioonyeshwa na WHO, GAVI na Taasisi zingine zinazounga mkono jitihada hizo,”amesema Dk Subi.

Alisema kwa kutambua ugonjwa huo umegharimu maisha ya watu wengi wanafanya tathmini ya ubora wa chanjo hiyo kabla ya kuikubali na kuanza kutumika nchini.

Mkutano huo unaofanyika kwa njia mbili ya ana kwa ana na video, umehudhuriwa na nchi zote Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kesho watakutana Makatibu Wakuu na Aprili 23, 2021 watakutana Mawaziri wanaosimamia masuala ya Afya kutoka nchi Wanachama.

Chanzo: www.habarileo.co.tz