Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EAC yapoteza Dola bil 4.8 janga la corona

67a1d2136013724f3523a0cdf1464aa8.jpeg EAC yapoteza Dola bil 4.8 janga la corona

Wed, 5 May 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

NCHI wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinakadiriwa kupoteza Dola za Marekani bilioni 4.8 katika mwaka 2020 zitokanazo na sekta ya utalii kutokana na janga la ugonjwa wa Covid-19.

Hayo yamebainishwa katika utafiti uliofanywa na Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) kwa msaada wa Jumuiya ya Utafiti wa Kiuchumi Afrika (AERC) na Bill na Melinda Gates Foundation kuhusu athari za COVID-19 kwenye eneo la utalii na ukarimu na chaguzi za sera kutokana na usumbufu wa COVID-19 na magonjwa ya mlipuko ya baadaye.

Akizungumza katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandaoni Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC), Dennis Karera alisema utafiti huo utachangia kukuza chaguzi za sera kukuza uchumi na utalii.

Alisema utafiti huo unaonyesha kuwa utalii ambao ulichangia wastani wa asilimia 9.5 katika Pato la Taifa mnamo 2019 na wastani wa asiliamia 17.2 kwa jumla ya usafirishaji wa EAC, lilikuwa moja wapo ya maeneo yaliyoathirika zaidi katika ukanda huo.

Utafiti huo pia ulionesha kuwa wageni katika hifadhi za kitaifa walipungua kwa karibu ya asilimia 65 na kuathiri vibaya juhudi za uhifadhi wa wanyamapori katika ukanda huo.

Aidha alisema utafiti ulipendekeza kwa maeneo ya utalii kuwa na maandalizi ya janga na mipango ya usimamizi wa hatari ili kupunguza madhara kama hayo kwa baadaye.

Kadhalika alisema ripoti hiyo inaeleza nia ya wadau wa utalii kutaka kudumishwa kwa vifurushi vya kichocheo vilivyotolewa na serikali za EAC ili kuainisha upya na kufafanua tena bidhaa za utalii kwa kutumia teknolojia za dijiti katika uuzaji na utangazaji wa utalii.

Chanzo: www.habarileo.co.tz