Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EAC yaipongeza Tanzania kwa amani

29522b28c43556c8a94e92fc322872dd EAC yaipongeza Tanzania kwa amani

Tue, 6 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SEKRETARIETI ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imepongeza serikali na wananchi wa Tanzania kwa kuendelea kudumisha na amani na kubadilishana madaraka kwa utulivu baada ya kifo cha Rais wa Tano wa Tanzani, John Magufuli.

Katika barua ya pongezi kwa Rais Samia Suluhu kwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania, sekretarieti hiyo imeeleza kuwa, mabadiliko ya madaraka yaliyofanyika kwa utulivu ni ushahidi wa utamaduni wa kidemokrasia, kikatiba na utawala bora uliopo Tanzania na ukanda huo.

Barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Liberat Mfumukeko imeeleza kuwa kubadilishana madaraka kwa amani ni ushindi siyo kwa Tanzania tu, bali Afrika Mashariki kwa ujumla.

“Jumuiya inatarajia Tanzania kuendelea na mchakato wa mtangamano wa Jumuiya ya Afrika MAshariki kwa kushirikiana na nchi nyingine wanachama,” alisema Katibu Mkuu huyo wa EAC katika barua hiyo.

Ikitoa salamu za rambirambi kwa msiba wa Rais Magufuli, EAC imeeleza kuwa Rais huyo ameacha urithi wa reli ya kisasa inayounganisha nchi za EAC. Reli hiyo inaanzia Bandari ya Dar es Salaam-MorogoroDodoma-Isaka-Mwanza, Isaka-Rusumo-Kigali (Rwanda) na Tabora-Uvinza-MusongatiGitega (Burundi).

Balozi Mfumukeko alisema Rais Magufuli alikuwa mwenye talanta na shujaa wa Afrika Mashariki ambaye siku zote hakutaka chochote ila ubora kwa nchi yake na Afrika.

“Alikuwa pia kiongozi shupavu mwenye uwezo usio na kifani wa kufanya kazi kwa bidii.” “ Magufuli alichukia ukabila, ufisadi, uchoyo na uvivu na uovu ambao umekuwa hatari kwa nchi nyingi za Kiafrika,” alisema Katibu Mkuu huyo wa EAC.

Alisema baada ya kuchukua madaraka kwa kushinda uchaguzi wa urais Oktoba 2015, Rais Magufuli alianza safari ya kuibadilisha Tanzania katika nyanja zote ikiwamo miundombinu, uzalishaji, kilimo, madini na mengineyo.

“Rais Magufuli alibadilisha shughuli katika Bandari ya Dar es Salaam ambayo ni moja ya njia kuu mbili kwa Afrika Mashariki kwa kuondoa rushwa na hivyo kuifanya kuwa yenye ufanisi mkubwa.”

“Aliongeza ukusanyaji wa mapato ya kitaifa na kuziba mianya ambayo ilisababisha upotezaji wa ushuru na hivyo kuipa serikali fedha zaidi za utoaji wa huduma kwa umma,” alisema.

Balozi Mfumukeko alisema Magufuli aliboresha utumishi wa umma kwa njia ambazo haziwezi kufikirika Afrika kwa kuwajenga watumishi kujua kwamba wananchi wa kawaida (raia) ndio waajiri wao halisi na hivyo wanapaswa kutoa huduma bora.

“Rais Magufuli aliacha alama katika nyadhifa zote alizoshika katika utumishi wa umma. Hapo awali akiwa Waziri wa Ujenzi alihakikisha serikali inajenga barabara nzuri kwa bei nafuu na kwa viwango vya juu kabisa,” alisema.

Chanzo: www.habarileo.co.tz