Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EAC kumkumbuka Magufuli kwa reli ya kisasa

85137ce3bf4fca824a051852cc282683.jpeg EAC kumkumbuka Magufuli kwa reli ya kisasa

Sat, 20 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SEKRETARIETI ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imemlilia Rais John Magufuli na kusema ameacha urithi wa ujenzi wa reli ya kisasa inayounganisha nchi za EAC. Reli hiyo kuanzia bandari ya Dar es Salaam na Morogoro-Dodoma-Isaka-Mwanza; Isaka-Rusumo-Kigali (Rwanda) na Tabora-Uvinza-Musongati-Gitega (Burundi).

Kutokana na Msiba huo,imetaka bendera zote katika vyombo na taasisi za EAC kupeperuka nusu mlingoti hadi Rais aliyefariki atakapozikwa.

Katibu Mkuu wa EAC, Balozi Libérat Mfumukeko aliyasema hayo katika barua yake kwenda kwa Rais Samia Hassan Suluhu na kueleza kusikitishwa kwa msiba wa Magufuli aliyekuwa Rais wa Tanzania, na mjumbe wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za EAC.

Alieleza Jumuiya imepoteza mshauri na kiongozi ambaye alitoa ushauri wa busara kila anapoombwa kufanya hivyo.

Rais Magufuli alikuwa mwenye talanta na shujaa wa Afrika Mashariki ambaye siku zote hakutaka chochote ila ubora kwa nchi yake na Afrika. Alikuwa pia kiongozi shupavu mwenye uwezo usio na kifani wa kufanya kazi kwa bidii.

“Kwa wale wote ambao walimpenda na kumheshimu Rais Magufuli, tunadeni ambalo ni kuyaenzi maono aliyokuwa nayo kwa nchi yake na EAC,”alisema Balozi Mfumukeo

Alisema EAC wanaomboleza kwa kumpoteza kiongozi huyu mashuhuri na ambaye alifanya mengi kwa Tanzania na Jumuiya kwa zaidi ya miaka mitano ambayo amekuwa madarakani.

“ Magufuli alichukia ukabila, ufisadi, uchoyo na uvivu, uovu ambao umekuwa hatari kwa nchi nyingi za Kiafrika”alisisitiza Katibu Mkuu wa EAC

Baada ya kuchukua madaraka kwa kushinda uchaguzi wa urais mnamo Oktoba 2015, Rais Magufuli alianza safari ya kuibadilisha Tanzania kwa kubadilisha katika Nyanja zote kwa kuongeza miundombinu, uzalishaji wa kilimo na utajiri wa madini.

Katibu mkuu huyo alisema Rais Magufuli alibadilisha shughuli katika bandari ya Dar es Salaam,ambayo ni moja ya njia kuu mbili kwa Afrika Mashariki kwa kuondoa rushwa na hivyo kuifanya bandari hiyo kuwa yenye ufanisi mkubwa.

Rais Magufuli alizidi kuongeza ukusanyaji wa mapato ya kitaifa kwa kuziba mianya ambayo ilisababisha upotezaji wa ushuru na hivyo kuipa serikali fedha zaidi za utoaji wa huduma kwa umma.

Balozi Mfumukeko alisema Magufuli alibainisha jukumu la utumishi wa umma kwa njia ambazo haziwezi kufikirika katika bara kwa kuwajengea wafanyakazi kwamba wananchi wa kawaida (raia) ndio waajiri wao halisi na kwa hivyo wanastahili utoaji huduma bora .

Alisema Magufuli daima aliwataka wafanyakazi wa ngazi yoyote kujiona kama watumishi wa wananchi kinyume na mabeberu .

“Rais Magufuli aliacha alama katika nyadhifa zote alizoshika katika utumishi wa umma. Hapo awali, akiwa Waziri wa Ujenzi , alihakikisha kuwa serikali inajenga barabara nzuri kwa bei nafuu na kwa viwango vya juu kabisa”alisistiza

Kwa hivyo Tanzania, ni mojawapo ya mitandao bora ya barabara sio tu katika eneo hilo lakini barani Afrika nzima, mtandao ambao bado unakua kila siku. Mtandao huu unaunganisha nchi na eneo lote la EAC na kwingineko.

Chanzo: www.habarileo.co.tz