Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EAC: Nchi wanachama kuongoza vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa

Eac Sudan.jpeg EAC: Nchi wanachama kuongoza vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Kenya, William Ruto amesema ni lazima hatua za kiubunifu na endelevu zibuniwe ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Hatua ambazo rais Ruto amesema zitachukuliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki wakati ikielekea Dubai kwa mkutano kuhusu mazingira wa COP28 baadaye mwezi huu.

Akizungumza katika kikao cha wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na usalama wa chakula jijini Arusha, Rais Ruto amemsea Afrika itatumia na kuonyesha uwezo wake katika mapambano dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Miongoni mwa viongozi wa nchi za EAC wanaohudhuria kikao hicho ni pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan (Tanzania), Evariste Ndayishimiye (Burundi) na Salva Kiir (Sudan Kusini).

Miongoni mwa viongozi wengine wanaohudhuria kikao hicho ni pamoja na waziri mkuu wa Rwanda Edouardo Ngirente Rebecca Kadaga, naibu waziri mkuu wa kwanza wa Uganda.

Aidha rais Ruto ameeleza kuwa Afrika itatoa wito wa kusainiwa kwa mkataba mpya wa ufadhili ambao utarekebisha mfumo wa sasa wa kifedha wa kimataifa, ambao hauendani na hali ya sasa ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Kenya, EAC na Afrika, alieleza, zinajenga muungano wa kimataifa utakaosaidia kuipa dunia mtazamo mapya ambayo utasaidia katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live