Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

EABC yatoa pole kifo cha Rais Magufuli

A2eeab66893a88d9acc45c86315e1e59 EABC yatoa pole kifo cha Rais Magufuli

Fri, 19 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

BARAZA la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limesema jamii ina wajibu wa kuenzi maono ya Rais John Magufuli kuhusu umoja, amani na maendeleo ya viwanda ili kukuza uchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Taarifa ya Ofisa Mtendaji Mkuu wa EABC, Dk Peter Mathuki ilieleza kuwa baraza hilo linaungana na wananchi na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa jana jijini Arusha, Mwenyekiti, bodi ya wakurugenzi, menejimenti na wanachama wa EABC wametuma rambirambi kwa familia, wananchi na serikali ya Tanzania kwa kufiwa na Rais Magufuli.

Mathuki alisema Magufuli alikuwa mwana Afrika kiongozi mzalendo aliyeanzisha maono ya ujenzi wa Tanzania ya viwanda, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), kufufua Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), na ujenzi wa mradi wa umeme katika Bwawa la Nyerere Rufiji.

Alisema maono ya Magufuli yaliwezesha maendeleo ya Watanzania na eneo la EAC. “Utumishi wake uliwezesha ukuaji wa uchumi na kuipandisha Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuwa na sifa ya nchi yenye uchumi wa kati” alisema Mathuki katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari.

Alisema wakati Magufuli akiwa Mwenyekiti wa wakuu wa nchi EAC alizindua na kuidhinisha kanuni za biashara EAC na kusisitiza nguvu za pamoja kupambana na rushwa katika eneo hilo.

Mathuki alisema, Magufuli alikuwa mstari wa mbele kuhimiza wajibu wa sekta binafsi katika mafanikio ya kiuchumi, alihamasisha maendeleo ya viwanja, miundombinu, na kukuza sekta ya nishati EAC sanjari na kuhamasisha matumizi ya bidhaa na hu

Chanzo: www.habarileo.co.tz