Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Donholm: Jamaa azirai na kufariki dunia mbele ya duka la kuuza pombe

0ea7ce7cd1f5db7b Donholm: Jamaa azirai na kufariki dunia mbele ya duka la kuuza pombe

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke

- Jamaa huyo anasemekana kufika katika duka la kuuza pombe mwendo wa saa tatu asubuhi lakini haijabainika iwapo alinunua vileo au la

- Kufikia saa saba mchana, alianguka na kuziran nje ya duka hilo

- Wahudumu wa afya walifika eneo la tukio na kunyunyizia mwili wake dawa kabla ya kuubeba na kuupeleka kwenye chumba cha kuhifadhi wafu

Maafisa wa polisi mtaani Donholm wanachunguza kisa kimoja ambapo jamaa mmoja alianguka na kuzirai mbele ya duka moja linalouza pombe.

Kwa mujibu wa taarifa za The Standard, jamaa huyo anasemekana alifariki dunia akiwa katika duka hilo lilofahamika kama Jawa Wines na spirit mwendo wa saa tatu asubuhi lakini haikubainika kama alikuwa amenunua vileo.

Dakika chache baadaye, maafisa wa polisi walifika katika eneo la tukio na kuunyunyiza mwili wake na dawa kabla ya kuusafirisharisha hadi katika chumba cha kuhifadhi wafu.

Ingawa kiini cha kifo chake hakikubainika kwa haraka, kulikuwa na madai kwamba huenda jamaa huyo aliangamizwa na virusi vya COVID-19.

Kwenye taarifa zingine, chifu mmoja alizirai na kufariki dunia akifanya mtihani wake wa kitaifa Machi 30, 2021.

liripotiwa kwamba Abdullahi Shurie alizirai Jumanne Machi 30, 2021 na kukimbizwa hospitalini lakini madaktari hawangeweza kuyaokoa maisha yake.

Kulingana na taarifa kutoka kwa wasimamizi wa mtihani, marehemu alikuwa akifanya mtihani wa somo la kemi kabla ya kukata roho.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia [email protected] au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama habari zaidi kutoka TUKO.co.ke

Chanzo: kiswahili.tuko.co.ke