Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dola laki 9 za misaada zaibiwa DRC

Zbimg 10033 800 Dola laki 9 za misaada zaibiwa DRC

Thu, 8 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika moja la misaada lenye makao yake makuu nchini Marekani, GiveDirectly, limesema kuwa takribani dola laki 900,000 ziliibiwa kutoka katika programu zake za nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

GiveDirectly ilisema kwamba iligundua kuwa watu katika timu yake ya Kongo walifanya kazi na watu nje ya shirika ili kulaghai mpango wa uhawilishaji fedha, na kuelekeza misaada kutoka kwa zaidi ya familia 1,700 masikini zaidi ya miezi sita, kuanzia Agosti 2022.

“Udanganyifu huu uliwezekana tu kwa sababu ya mabadiliko maalum tuliyofanya katika mchakato wetu wa malipo ili kufanya kazi katika eneo hili la mbali, lisilo salama la (Kongo),” kulingana na taarifa kutoka Jumatatu.

“Tunajuta sana kwa kutopata hili mapema na kuchukua kwa uzito udhaifu uliofichua,” ilisema.

Zaidi ya familia 1,700 maskini ambazo zilihitaji misaada zimeathirika na wizi huo uliotendeka kwa kipindi cha zaidi ya miezi sita kuanzia mwezi Agosti mwaka 2022.

Uchunguzi unafanyika ili angalau kurejesha sehemu ya fedha hizo ingawa kiasi kikubwa cha pesa hiyo huenda kisipatikane.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live