Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dola bilioni 1.4 zahitajika kusaidia wakimbizi Sudan Kusini

Sudan Kusini Uchumi Kuzorota Dola bilioni 1.4 zahitajika kusaidia wakimbizi Sudan Kusini

Sun, 31 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) na washirika wametoa wito wa msaada wa dola bilioni 1.4 za kimarekani katika mwaka 2024, ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi milioni 2.3 wa Sudan Kusini walioko katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ethiopia, Kenya, Sudan na Uganda kupitia mtaji mpya.

Mkurugenzi wa UNHCR kanda ya Afrika Mashariki, Pembe ya Afrika na Maziwa Makuu Mamadou Dian Balde, amesema katika muongo uliopita, kumepatikana maendeleo makubwa yanayoonekana kidhahiri kwa wakimbizi waliopata misaada. Amesema iwapo rasilimali itapatikana, msaada wa kibinadamu wa uwekezaji kwa wakimbizi na jamii utawezesha kupatikana utatuzi wa muda mrefu wa matatizo yaliyopo.

Katika taarifa iliyotumwa kwenye tovuti yake, UNHCR ilisema "Tangu kuanza kwa mzozo nchini Sudan Kusini zaidi ya miaka 10 iliyopita, kuongezeka kwa mahitaji ya kibinadamu hasa uhaba mkubwa wa chakula, ukosefu wa usalama endelevu, na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, kumewasabishia matatizo wakimbizi wa Sudan Kusini ."

Taarifa hiyo iliongeza kuwa miaka minne mfululizo ya mafuriko "pia yameharibu nyumba na maisha, na kupelekea watu wengi wa Sudan Kusini kukimbilia nchi jirani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live