Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dkt. Mpango afungua Mwaka Mpya wa mahakama ya Afrika

Dkt Phillip Mpango Xmass.jpeg Dkt. Mpango afungua Mwaka Mpya wa mahakama ya Afrika

Tue, 21 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameitaka mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) kuendeleza majadiliano na Nchi za Kiafrika ili kuongeza wigo wa mataifa hayo kuruhusu wananchi wake kuepeleka mashauri kwenye mahakama hiyo.

Dkt. Mpango ametoa kauli hiyo wakati akifungua Mwaka Mpya wa mahakama ya Afrika, hafla ambayo imefanyika katika makao Makuu ya mahakama hiyo yaliyopo jijini Arusha.

Amesema majadiliano hayo yatasaidia kuondoa dhana ambayo imejengeka kwenye mataifa ya Afrika Kuwa mahakama hiyo imekua ikiingilia uhuru wa mataifa Yao licha ya kuridhia uanzishwaji wake mwaka 2006 jijini Addis Ababa.

Aidha ameongeza Kuwa Serikali ya Tanzania itaendelea kuhakikisha utangamano wa Mahakama hiyo unaendelea kukua kulingana na kusudi la uanzishwaji wake.

Awali akimkaribisha Dkt. Mpango, Rais wa Mahakama ya Afrika Jaji Imani Aboud amesema tangu kuanzishwa Kwa mahakama miaka 16 iliyopita imetoa maamuzi zaidi ya 200 ya mashauri mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika yakihusu masuala nyeti ya kijamii, kisiasa na kiuchumi yanayowakilisha maisha ya Kila Siku ya Waafrika wa kawaida.

Jaji Aboud ameongeza Kuwa wanaoendelea na majadiliano na mataifa mengine ili kuongeza upana wa kiutendaji wa Mahakama huku pia akibainisha Kuwa nchi wanachama katika ngazi ya kitaifa Zina jukumu la kulinda Haki za Binadamu Kwa Kuwa mahakama ya Afrika haiwezi kuchukua jukumu hilo la ndani.

Kati ya nchi 55 za Afrika ni nchi 33 zilizoridhia itifaki ya kuanzishwa kwa mahakama hiyo, ambapo nchi 8 tu zimetoa tamko la kuwaruhusu wananchi wake na taasisi za kiraia kupeleka mashauri yao moja kwa moja katika mahakama hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live