Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Diane Rwigara aenguliwa tena ugombea Urais Rwanda

Mtoto Wa Kagame Aenguliwa Tena Ugombea Urais Rwanda Diane Rwigara aenguliwa tena ugombea Urais Rwanda

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matumanini ya mpizani wa Rais Paul Kagame, Diane Rwigara kugombea urais katika uchaguzi wa Julai 14, 2024 yameyeyuka baada ya Tume ya Uchaguzi ya Taifa ya Rwanda (NEC) kuliondoa jina lake kwenye orodha ya wagombea.

Ni wagombea watatu tu kutoka uchaguzi wa urais wa 2017 waliopatikana kwenye orodha ya muda ya wagombea iliyotolewa na NEC jana Alhamisi, Juni 6, 2024.

Miongoni mwa wagombea hao, yuko Rais Paul Kagame, anayeendelea kutetea nafasi hiyo tangu nchi hiyo ilipotoka kwenye mauaji ya kimbari mwaka 1994.

Wagombea wengine ni Frank Habineza wa Chama cha Kijani na mgombea huru Phillippe Mpayimana.

Uamuzi wa kumwengua Rwigara (42) utakuwa pigo kubwa kwa mwanaharakati huyo ambaye ni mtoto wa aliyekuwa mfadhili wa zamani wa Chama cha Rwanda Patriotic Front (RPF), Assinapol Rwigara, aliyeuawa katika ajali ya gari iliyoacha utata Februari 2015.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa NEC, Oda Gasinzigwa amesema Rwigara ameshindwa kuwasilisha mahitaji kama vile rekodi ya uhalifu na kulikuwa na kasoro kadhaa kwenye saini zinazomuunga mkono.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live