Afrika

Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dhahabu yapelekea mauaji watu 13 Mgodini

Maafisa Wa Jeshi Wasema Wamechukua Mamlaka Gabon Dhahabu yapelekea mauaji watu 13 Mgodini

Wed, 30 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Msemaji wa Jeshi na Kiongozi wa Mashirika ya Kiraia, Dieudonne Lossa amesema Watu wasiojulikana, wakiwa na Silaha wamewauwa watu 13 kwenye machimbo ya Dhahabu katika eneo la Mashariki mwa nchi yas Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo – DRC.

Shambulio hilo, lilnadaiwa kutekelezwa majira ya usiku katika eneo hilo ambalo pia lipo jirani na machimbo ya madini ya Shaba yanayomilikiwa na watu binafsi huko Aru, karibu na mpaka kati ya Uganda na jimbo la Ituri.

Alisema, “Watu kumi na watatu wameuawa, tisa wamejeruhiwa vibaya na wengine kadhaa kuchukuliwa mateka na washambuliaji nadhani watu hao walilenga kupoka na kusafirisha dhahabu na bidhaa zao nyingine walizoziiba.”

Alisema kuwa makundi mawili yenye silaha yanafanya harakati zao katika eneo hil ambayo ni Ushirika wa Maendeleo ya Congo – CODECO na Wanamgambo hasimu wanaoitwa Zaire, wakiwa ni miongoni mwa makundi ya wanamgambo wanaoendesha shughuli zao katika eneo la Mashariki, lililogubikwa na migogoro.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live